Sheria ya ugavi wa rasilimali za madini kufanyiwa mabadiliko

titanium_mining_kenya

Waziri wa madini Dan Kazungu ameahidi kuwa sheria kuhusu ugavi wa rasilimali za madini itafanyiwa mabadiliko katika kipindi cha miezi 3 ijayo.

Akizungumza alipozuru migodi ya uchimbaji madini ya Base Titanium kaunti ya Kwale,Kazungu amesema sheria ya sasa ilipitishwa mwaka wa 1940 na haimfaidi mwananchi na hata taifa kimapato hivyo ipo haja ya kufanyiwa marekebisho.

Amesema sekta ya madini inachangia asilimia moja pekee ya uchumi wa taifa hili licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa madini unaomfaidi mwekezaji,huku taifa likisalia na asilimia chache pekee.

Ameahidi kutatua asilimia 80 ya mizozo inayoshuhudiwa kati ya serikali za kaunti, wananchi na waekezaji wa uchimbaji madini ili kuipa sekta hiyo umuhimu wa kuinua uchumi wa taifa hili.

https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287