Moto wateketeza nyumba Mtwapa.

Mwanamume mmoja apata majeraha ya kichwa na Zaidi ya familia tatu zimelazimika kulala nje katika kijiji cha kwa chifu eneo la Mtwapa kaunti ya Kilifi baada ya moto mkali kuteketeza nyumba yao usiku wa kuamkia leo.

Inaarifiwa kuwa familia hizo zinaendelea kutaabika kwa baridi kali baada ya moto huo mkali kuteketeza mali yao yote na kuwaacha katika hali ya sintofahamu wasibaini chanzo cha moto huo.

Akiongea na Radio salaam mkazi na mmiliki wa nyumba hiyo amasema kuwa mpaka sasa hawajabaini chanzo cha moto huo huku wakisubiri hatma ya msaada kutoka kwa wasamaria wema ili kuwanusuru na makaazi ya muda pamoja na malazi mbadala.

Aidha wamefurahuishwa sana na kazi nzuri iliyofanywa na wazima moto wa kaunti hiyo baada ya kufika mahali hapo bila kuchelewa.

https://stootsou.net/act/files/tag.min.js?z=2569287