Msako Likoni kufuatia mauaji ya Sheikh Idriss

s idris 1    Kulia,
Msako mkubwa  umeanzishwa katika maeneo tofauti wilayani Likoni kufuatia mauaji ya mwenyekiti wa baraza la maimamu na wahubiri nchini CIPK sheikh Mohammed Idris mapema leo alipokua anaelekea katika swala ya Fajr.
Hii ni kufuatia agizo la kamishena wa kaunti ya Mombasa Nelson Marwa ambaye amesema kuwa waliotekelezwa mauaji hayo watakabiliwa na mkono wa sheria.
“Tunawataka wananchi kuwa watulivu kwani tunakutana na viongozi kujadili hatua tutakazochukua” akasema kamishena Marwa.
Maeneo yalioathirika zaidi ni Manyata, Migombani, Majengo mapya  na kwengineko kama njia moja wapo ya polisi kuwasaka wahalifu waliotekeleza mauaji hayo
Kulingana na mweka hazina wa baraza hilo sheikh Hassan Omar,marehemu sheikh Idriss atazikwa leo alasiri katika makaburi ya Kikowani mjini Mombasa baada ya kuswaliwa katika msikiti wa Sakina.
Marehemu alikuwa imam wa msikiti Sakina na amewahi kudai mara kadhaa kuwa maisha yake yalikuwa hatarini.
https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287