Serikali yaanzisha msako kuwatafuta waliotekeleza mauaji ya sheikh Idriss

Kamishena wa kaunti ya Mombasa Nelson Marwa ametoa wito wa utulivu huku serikali inapochunguza mauaji ya Sheikh Mohammed Idriss aliyeuawa mapema leo eneo la Likoni kaunti ya Mombasa.

Marwa amesema kuwa tayari polisi wameanzisha oparesheni kuwasaka waliohusika na akatoa wito kwa yeyote mwenye habari zitakazosaidia polisi na uchunguzi kuziwasilisha.
“Tunawataka wananchi kuwa watulivu kwani tunakutana na viongozi kujadili hatua tutakazochukua” akasema kamishena Marwa.
Marwa ametoa hakikisho kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuwakamatwa wahusika ili wakabiliwe na mkono wa sheria.