kuppet kwenda mahakamani

CHAMA cha walimu cha KUPPET kimeahidi kwenda mahakamani siku ya jumatatu wiki ijayo kuwatetea walimu wa kaunti ya Garisa, Mandera na Wajir ambao wamegoma kurudi kazini kwa madai ya utovu wa usalama katika maeneo hayo.

Kulingana na mwenyekiti wa KUPPET Omboko Milemba ni kuwa serikali inapaswa kuacha kuwatishia maisha walimu kwa kuwafuta kazi na badala yake watafute suluhu ya kudumu itakayo saidi pande zote mbili.

Milemba aidha amedokeza kuwa tayari chama hicho kimeipa maelezo kampuni ya mawakili ya JUDITH Buswero kuwawakilisha mahakamani ikiwa lengo kuu ni kusimamisha hatua ya serikali kupitia tume ya kuajiri walimu ya TSC kuwafuta wlaimu hao

https://stootsou.net/act/files/tag.min.js?z=2569287