Bunge kurejelea vikao baada ya likizo fupi

bungeBunge linarejelea vikao vyake leo baada ya likizo fupi ya mwezi mmoja.

Wabunge watakuwa na orodha ndefu ya maswala ambayo watajadili katika kipindi hiki miongoni mwao ikiwa ni hoja ya kumuondoa mamlakani waziri wa maswala ya ugatuzi Ann Wiguru.
Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Adan Duale amesema kuwa juhudi zinaendelea kumshawishi mbunge wa Igembe kusini ambaye amewasilisha hoja hiyo bungeni kuiondoa.
Wabunge wa chama cha TNA wanapanga kukutana asubuhi ya leo kabla ya vikao vya bunge kufunguliwa baadaye leo.
Maswala mengine yatakayopewa kipau mbele ni ripoti za kamati za bunge moja ikiwa ile iliyochunguza sakata ya reli na ile iliyochunguza sakata ya anglo-leasing.
https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287