Viongozi wakutana kwa maombi

nyatta

 

 

 

 

Viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamejumuika pamoja na viongozi wengine kutoka tabaka mbali mbali katika hoteli ya safari Park jijini Nairobi kwenye mkutano wa maombi kwa taifa.

Mkutano huo huandaliwa na bunge na hufanyika kila mwaka ili kuliombea taifa hili kutokana na changamoto zinazolikabili.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mkutano huo ni wabunge, maseneta, mawaziri na viongozi wengine kutoka maaifa ya nje.

Haya yanajiri huku Kenya likishuhudia utovu wa usalama, madai ya ukabila na ufisadi.

Hatua hii ya maombi ni njia mojawapo ya kuwaleta viongozi wa serikali na wa upinzani pamoja na kusaka suluhisho juu ya matatizo ya Wakenya.

https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287