Polisi watuhumiwa kwa kutekeleza mauaji ya kiholela Mombasa

police upload
Familia za vijana wawili waliouawa na maafisa wa polisi jana asubuhi kwa madai ya kuwa majamabazi katika mtaa wa Hongera wilayani Kisauni wamekashifu mauwaji hayo na kuyataja kuwa ya kiholela.
familia ya mmoja wa vijana aliyeuwawa, Ali Rashid, inadai kusikitishwa na mauaji ya Kijana huyo mwenye umri wa miaka 16 huku ikiilaumu polisi kwa kumuua bila sababu.
Polisi walisema kuwa vijana hao walikuwa majambazi waliowahangaisha waakazi wa Kisauni.
Familia hiyo imesema kuwa kijana huyo alipigwa risasi licha ya kusalimu amri na kuonyesha kuwa hakuwa na hatia.
Wakati huo huo seneta maalum kutoka kaunti ya Mombasa Emma Mbura ameitaka idara ya usalama kuingilia kati na kusitisha mauwaji hayo ya kiholela.
Vile vile mtetezi mkurugenzi kutoka shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Africa Hussein Khalid ameitaka serikali kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika katika mauwaji hayo.
https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287