Mahakama ya Rufaa yasimamisha kukamatwa kwa mwanahabari Walter Barasa

Ni afueni kwa mwanahabari Walter Barasa baada ya mahakama ya rufaa kusitisha kwa muda agizo la kukamatwa kwake na kupelekwa katika mahakama ya kimataifa ya jinai ICC lililotolewa na mahakama kuu, hadi kesi yake itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Walter-Osapiri-Barasa

Hii ni baada ya Barasa kuwasilisha kesi katika mahakama ya rufaa baada ya mahakama kuu kutoa agizo la kukamatwa na kupelekwa katika mahakama ya ICC.
Barasa anadaiwa kuwahonga mashahidi hivyo basi kuingilia ushahidi wa mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo Fatou Bensoda.
Hii ni mara ya pili kwa mwanahabari huyo kwenda mahakamani akitaka kuzuia jaribio lolote la kumkamata na kumkabidhi kwa mahakama ya ICC.
Na Asha Bekidusa
https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287