Gavana wa Kericho afika mbele ya Bunge la Seneti kujibu Shutma dhidi yake

Gavana wa Kericho aliyetimuliwa na bunge la kaunti Paul Chepkwony amekufika mbele ya kamati ya bunge la seneti ili kujibu madai yaliyowasilishwa na bunge la kaunti hiyo mbele ya bunge la seneti.
Gavana huyo amesema kuwa yuko tayari na amejiandaa kujibu madai hayo kwa kutumia ushahidi wa stakabadhi dhidi ya madai hayo.
Hatma ya gavana huyo sasa iko mikononi mwa kamati hiyo ambayo inafanya vikao vyake katika ukumbi wa KICC.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Dr. Chris Obure amesema kuwa kamati yake itawasilisha ripoti yake katika bunge la seneti jumanne ya wiki ijayo.
Chepkwoni anatuhumiwa kwa kukiuka katiba kuhusiana na usimamizi wa fedha za umma na utumiaji mbaya wa mamlaka.
https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287