Polisi waruhusu mkutano wa Cord wa jumamosi ufanyike

CORDmeet301013

Viongozi wa mrengo wa Cord sasa wanasema kuwa wamekubaliwa kuandaa mkutano wao wa siku ya jumamosi ili kumkaribisha kinara wao Raila Odinga katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi.

Hii ni baada ya Inspekta Jenerali wa polisi David Kimaiyo kubadili msimamo wake kuhusu marufuku iliyotangazwa jana dhidi ya mikutano yote ya kisiasa humu nchini.
Katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga humu nchini jumanne usiku, Kimaiyo alisema kuwa anapanga kukutana  na viongozi wa kisiasa ambao wameandaa mikutano yao mwishoni mwa juma hili, ili kulijadili suala hilo.
Siku ya jumanne Idara ya polisi ilitangaza kupiga marufuku mikutano yote ya kisiasa kutokana na kile ilichosema ni sababu za kiusalama.
Hatua hiyo ilizua hisia mseto huku mirengo ya Cord na Jublee ikiapa kuendelea na mikutano yao inayopangiwa kufanyika mwishoni mwa wiki.
Wanacord wanapanga kukutana katika uwanja wa Uhuru, jijini Nairobi, huku wenzao wa Jubilee wakikutana mjini Kajiado.
https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287