Maafisa wawili wa KDF wauawa na washukiwa wa Al-shabab huko Lamu

Maafisa wawili wa jeshi wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika  kaunti ya Lamu baada ya washukiwa wa kundi la wapiganaji nchini Somalia la Al-Shaabab kuushambulia msafara wao.
Maafisa hao wa kijeshi walikuwa wakisafirisha chakula kutoka Hindi hadi katika kambi yao katika eneo la Ras Kamboni na Lamu.
Afisa mkuu wa polisi wa Lamu mashariki Samuel Obara amethibitisha kisa hicho na kuongeza kuwa, maafisa hao walivamiwa na kundi la watu 10 katika msafara wao na kuwauwa maafisa hao wawili na kujesruhi wengineo.
Mkuu huyo wa polisi amefichua kuwa gari la jeshi lilikuwa limekwama katika eneo la kati ya Milimani na Mangai na Buasuba tatribani kilomita 21 kutoka Hindi kabla ya kuvamiwa na kundi hilo na ufyatulianaji wa risasi ukaanza.
Afisa huyo amesema kuwa maafisa zaidi wa usalama wametumwa katika eneo hilo kuwasaka majambazi hao.
Na Kauli Mwatela

 

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287