Polisi Mombasa wamhoji nduguye Abdul Malik anayezuiliwa Guantamo Bay kwa tuhuma za ugaidi

Ndugu wa mshukiwa wa ugaidi kutoka Kenya anayezuiliwa katika gereza la Guatanamo Bay nchini Cuba Abdulmalik Mohammed amesema kuwa anahofia maisha yake baada ya kutakiwa kufika katika kituo cha polisi kuandikisha taarifa.

Salim Khamis Khamsin anadai kuwa maafisa wa polisi kutoka kaunti ya Mombasa walimchukua usiku wa kuamkia leo alipokuwa eneo la Shelly Beach Likoni na marafiki zake na kumpelekea kituo cha polisi cha Likoni kumuhoji.

Khamsin anadai kuwa polisi hao waliweza kuingia nyumbani kwake na kupekua kabla ya kuchukua picha za kakake Abdulmalik pamoja na kuchukua gari lake.

Wakati huo huo dadake Khamsin, Mwajuma Rajab amesemma kuwa anahofia huenda maisha ya familia yake iko hatarini hasa baada ya kaka yao kutiwa mbaroni na kusafirishwa hadi gereza la Guantanamo Bay.

Hata hivyo mkuu wa polisi wilayani Likoni Robert Mureithi amesema kuwa maafisa wa polisi hawakuondoka na kitu chochote na kuongeza kuwa wanamhoji lakini hawajamkamata kwa madai yoyote.

Na Asha Bekidusa

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287