Mwanaharakati Moses Kuria Ahojiwa na tume ya Uwiano kwa tuhuma za Uchochezi

Mwanaharakati Moses Kuria amehojiwa leo na maafisa wa tume ya uiano na na utangamano kufuatia tuhuma za uchochezi.

Kuria anatuhumiwa kutumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook kuandika maandishi ambayo yanawachochea wakenya dhidi ya jamii fulani.
Mwanaharakati huyo wa TNA aliandamana na mawakili wake na kuhojiwa kwa zaidi ya masaa manne.
Kamishena wa tume ya NCIC Kyalo Mwenzi amesema kuwa tume hiyo ilimuagiza Kuria kufika mbele yake ili kutoa ufafanuzi kuhusiana na maandishi aliyoyaweka kwenye ukurasa wake wa facebook.
Mwenzi amesema kuwa watafanya uchunguzi wa kina kabla ya kutoa mapendekezo kwa afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko, endapo Kuria anapaswa kushtakiwa.
Tum ya NCIC kadhalika inasemekana kuwaandikia barua baadhi ya viongozi wa muungano wa cord kuwataka kufika mbele yake kujibu tuhuma za uchochezi.
Na Radio Salaam