Wanasiasa wa Bonde la Ufa wamtaka Duale kumuomba msamaha mbunge Alfred Keter

Viongozi wa mrengo wa Jubilee wanaendelea kugawanyika kuhusiana na suala la jaribio la kumtimuwa waziri wa ugatuzi Ann Waiguru.
Wabunge watatu kutoka bonde la ufa sasa wanamtaka kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Adan Duale kumuomba msamaha mbunge wa Nandi Hills Alfred Keter pamoja na wakaazi wa eneo bunge hilo kutokana na kile wanachokiita kutoa matamshi ya kumdhalilisha.
Duale amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akimuita Keter bubu akiwa na maana kuwa hajawahi kuzungumza bungeni tangu achaguliwe.
Hata hivyo wabunge hao Julius Melly wa Tinderet, Elijah Lagat wa Chesumei na wanaharakati wa ODM  David Songok na Kipkorir Menjo wameyataja matamshi ya Duale kama kumkosea heshima Keter na watu wa Nandi Hills huku wakimtaka kumuomba msamaha.
Kadhalika wamemtaka Duale kuwaomba msamaha walemavu kwa kuwakejeli mabubu.
Na Radio Salaam
https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287