Afisa wa ardhi akamatwa Taita Taveta kwa kuitisha hongo

Maafisa kutoka tume ya kupambana na ufisadi nchini katika kanda ya pwani wamemtia mbaroni afisa mmoja anayeshughulikia maswala ya ardhi katika kaunti ya Taita Taveta kwa kuhusika na ufisadi.

Mkurugenzi wa tume hiyo katika kaunti Ya Mombasa, Hassan Khalid amesema kuwa afisa huyo anayehusika na kupima na ugavi wa ardhi katika maeneo ya  Maungu, Buguta na Kasighau amekamatwa baada ya kuitisha hongo ya shillingi elfu 30 na hatimaye kupewa shillingi elfu kumi.
Khalid amesema kuwa mshukiwa huyo atafikishwa mahakamani siku ya Jumatano baada ya kushauriana na afisi ya mkurugenzi wa mashataka ya umma nchini Keriako Tobiko.
Na Solomon Zully
https://stootsou.net/act/files/tag.min.js?z=2569287