Washukiwa watatu wa ugaidi wasakwa na maafisa wa polisi

KENYA POLICEMaafisa wa polisi katika kaunti ya Mombasa wanawasaka washukiwa watatu wa ugaidi ambao wanadaiwa kuwa wana njama ya kutekeleza mashambulizi katika kanda ya pwani.

Duru kutoka kwa idara ya polisi zinaarifu kuwa watatu hao wanahusishwa na jaribio la shambulizi la gurunedi siku ya alkhamisi katika barabara ya Biashara katika kaunti hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa idara ya upelelezi katika kaunti ya Mombasa,Henry Ondiek amesema kuwa wanawasaka watatu hao ambao walitoweka baada ya kukamatwa na polisi huku mmoja wao akiwa amevalishwa pingu.

Kamishna wa kaunti ya Mombasa, Nelson Marwa aidha amewahakikishia wananchi usalama wao na kusema kuwa wanafanya kila juhudi ili kuwatia nguvuni washukiwa hao wa ugaidi ambao walitoroka baada ya kurusha kilipuzi.

Afisa mmoja wa polisi na Raia mmoja walijeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo na wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali moja mjini Mombasa.

Haya yanajiri wakati ambapo taifa la uingereza na Marekani wametoa tahadhari kwa raia wao kutozuru humu nchini kufuatia hofu ya shambulizi la Kigaidi.

 

Na Solomon Zully

 

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287