Taharuki Mombasa baada ya jaribio la shambulizi la Grunedi

Police lineUsalama umeimarishwa mjini Mombasa kufuatia shambulizi la grunedi alkhamisi usiku lililowalenga maafisa wa usalama.

Watu wawili miongoni mwao afisa wa polisi wanauguza majeraha kufuatia shambulizi hilo lililotekelezwa katika eneo la Mwembe Kuku barabara ya Biashara mjini Mombasa

Kulingana na polisi, mshukiwa mmoja alikuwa ametiwa mbaroni katika eneo hilo kabla ya mshukiwa wa pili kuibuka na kuwarushia kilipuzi na kumjeruhi raia mmoja na afisa wa polisi.

Kamishena w kaunti ya Mombasa Nelson Marwa amethibitisha kua washukiwa wawili wanazuiliwa na polisi kuhusiana na shambulizi hilo.

Gavana Hassan, Ali Joho seneta Hassan Omar na mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir walikuwa miongoni mwa viongozi waliofika kwenye eneo la tukio alkhamisi usiku.

Na Solomon Zullysal

https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287