Serikali ya Kaunti ya Kwale yanunua pampu mbili za maji

mwabudzo

Wakazi wa kiaunti ya Kwale wanakila haki ya kutabasamu baada ya serikali ya kaunti hiyo kununua pampu mbili za kusambaza maji safi zilizogharimu takriban shilingi milioni sita na laki tano.

Akizungumza wakati wa kupokea pampu hizo waziri anayeshughulikia maswala ya maji katika kaunti hiyo Hemed Mwabudzo amesema kuwa maeneo ya Kwale ni maeneo yanayoshuhudia uhaba wa maji licha ya kuwa ndio makao makuu ya serikali ya kaunti hiyo kutokana na hitilafu za pampu zilizopo kwa sasa hivyo kununuliwa kwa pampu hizo mpya zilizo na uwezo wa kusambaza maji ya kiasi cha cubic mita 55 kwa kila jisaa jimoja kuanlenga kutatua shida hiyo.

Aidha Mwabudzo amesema kuwa serikali hiyo inamipango ya kununua majenereta mawili ili kuweza kuhakikisha kuwa usambazaji wa maji hautosita pindi umeme utakapopotea katika maeneo hayo.

pampupicpic

 

Na Ummi Masoud

 

https://stootsou.net/act/files/tag.min.js?z=2569287