Magari kadhaa yanaswa  jijini Nairobi.

tintedZaidi ya magari 100 yamekamatwa na polisi karibu na eneo la Yaya Centre jijini Nairobi kwa kuwa na vioo vyeusi almaarufu ‘tinted’.

Hii ni kufuatia agizo la inspekta generali wa polisi David Kimayo  aliyesema kuwa hatua hiyo ni katika kuimarisha usalama nchini.

Kimaiyo  amesema kuwa sheria  ina athiri magari ya umma pekee kwani sheria ya inasisitiza magari ya umma hayapaswi kuendeshwa na vioo hivyo.

Kupitia msemaji wa polisi wa utawala Madoud Mwinyi idara hiyo imesema kuwa itaendeleza msako wa magari hayo hadi pale magari yote yatakapo ondoa vioo hivyo.

Na Asha Bekidusa

 

https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287