Mvua Kubwa yasababisha hasara nchini.

floodsMvua kubwa inayoendelea kunyesha kote nchini imesababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu kote nchini.

Sehemu zilizoathirika pakubwa na mvua hiyo ni barabara ambapo madaraja mengi yamesombwa na maji huku baadhi ya mapaa ya shule kadha nayo akisombwa na upepo.

Wakiongea na Radio Salaam, wakazi wa wilaya za Kwanza na Saboti katika kaunti ya Trans-Nzoia wamefichua kuwa imekuwa ni shida kwa wao kufika mjini Kitale kwa sababu ya barabara mbovu.

Wakulima wamaziwa akiongozwa na Pius Mzee Arap Kauka wamesema kuwa imekuwa nivigumu kwa wao kupeleka maziwa yao katika kiwanda cha maziwa cha new KCC  mjini Kitale kwa sababu barabara hazipitiki.

Maeneo mengine ambayo ameathiriwa na Mvua kubwa ni Kiplombe katika kaunti ya Uasin-Gishu, Morokojiti wilayani West-Pokot na Gitwamba wilayani Mlima-Elgon.

Na Juma Kauli Mwatela

 

 

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287