MSHUKIWA WA UJAMBAZI AUWAWA UKUNDA

Polisi maeneo ya Diani wampiga risasi na kumuua jambazi mmoja usiku wa kuamkia leo aliyekua miongoni mwa majambazi wengine wawili waliokuwa
wamejihami na bunduki wakijaribu kuvamia nyumba ya mtalii mmoja raia wa
uwizi katika eneo la ukunda.
Akizungumza na wanahabari afisa mkuu wa polisi wa Mswambweni Joseph Omija amesema kuwa waliarifiwa tarifa hizo na wananchi kuhusiana na jaribio la wizi kwa makaazi ya mtalii huyo hatua ambayo iliwalazimu kuchukua hatua za haraka.
Omija amesema kuwa mshukiwa aliyeuwawa hakupatikana na stakabadhi zozote za kuthibitisha anakotoka na kuendelea kuwa huenda akawa miongoni mwa wahalifu wanaomiliki bunduki ya aina AK47 kutokana na maganda ya risasi yaliyopatikana katika eneo la tukio.
Mwili wa mwendazake huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya eneo la pwani huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

 

Na Ummi Masoud

https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287