Nauli ya usafiri kushuka.

Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa matatu nchini Simon Kimutai amesema kuwa wako tayari kupunguza nauli ya matatu kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta kote ulimwenguni.

Katika kikao na waandishi wa habari jijini Nairobi, Kimutai amesema kuwa watafanya kikao na wamiliki wote wa matatu ili kulijadili swala hilo kwa kina.

Hata hivyo Kimutai ameikashifu vikali Tume ya Kudhibiti kawi nchini kwa kukosa kupunguza bei ya mafuti ili iweze kulingana na bei ya Ulimwengu mzima.

https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287