Uhaba wa damu

Wananchi wametakiwa Kujenga tamaduni ya kutoa damu haswa katika hospitali kuu na za mikoa humu nchini ili kuepuka upungufu wa bidhaa hiyo muhimu.

Akiongea na radio salaam waziri wa afya kaunti ya Mombasa Binty Omar ameeleza kuwa licha ya kuwa jukumu hilo ni la serkali ya kitaifa, kaunti ya Mombasa inapanga kuandaa mazoezi kadhaa ya kuhamasisha wananchi kutoa damu hasa wakati huu ambao hospitali kuu ya kanda ya pwani maarufu kama makadara inakumbwa na uhaba mkubwa wa damu na kutatiza shughuli tofauti za matatibabu ikiwemo kuzalisha na upasuaji.
Wakati huohuo Binty amewaaahidi wakaazi wa kaunti ya Mombasa na kanda ya pwani kwa ujumla kuwa wizara yake imeingia katika mazungumzo na wakurugenzi wa hospitali hiyo ilikuona ni vipi watashirikiana kutatua matatizo ya hospitali ya Makadara ikiwemo tatizo la uhaba wa damu na maji safi.

https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287