POLISI TISA WASIMAMISHWA KAZI KWA UZEMBE

IGKatika hatua inayoonekana ni ya kujaribu kurejesha nidhamu katika idara ya polisi, Inspekta Jenerali David Kimaiyo amewasimamisha kazi maafisa 9 wa polisi katika kaunti 3.
 Afisa mkuu wa kituo cha polisi cha Londiani kaunti ya Kericho Julius Mwarisi, maafisa 3 wa kitengo cha jinai na mmoja wa kikosi cha kupambana na mihadarati wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuhusika na njama ya kutoweka kwa misokoto elfu 2 ya bangi iliyokua imenaswa.
Kadhalika afisa mkuu wa polisi wilayani Wajir Kusini, Paul Munene na maafisa 2 wa Polisi wa Utawala katika kaunti ya Wajir wamesimamishwa kazi kwa madai ya kuhusika na njama ya kutoweka kwa magunia 147 ya sukari iliyoingia nchini kinyume cha sheria.
Shoka hilo pia limemuangukia afisa wa mwengine, John Ndhiwa wa kituo cha polisi cha Kanyiriri kaunti ya Kiambu, kwa tuhuma za kutumia bunduki yake kinyume cha sheria, hatua iliyopelekea kujeruhiwa kwa wananchi 3 wasiokua na hatia.
Kimaiyo amesema kwa sasa maafisa hao wanafanyiwa uchunguzi ili kubaini hatma yao.
Radio Salaam News desk
www.salaamfm.com
https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287