Sheikh Said Rageah aongoza Kongamano la kimataifa la kiislamu mjini Mombasa

Rageh
Kongamano la kimataifa la amani linalo ongozwa na mhubiri wa kiislamu kutoka nchini Canada, Sheikh Said Rageah limeanza rasmi mjini Mombasa huku maelfu ya watu mbali mbai wakijitokeza.
Kongamano hilo lililoandaliwa na Radio salaam na washikadau wake, linalenga kuuhamasisha umma na hususan waislamu juu ya uhuhimu wa kuimarisha amani na uwiano kati ya tabaka mbalimbali kwa minajili ya ya maendeleo ya jamii yoyote au nchi ulimwenguni.
Skeikh Said Rageah ambaye ni Mhadhir mkuu na msomi wa kimataifa , atakuwa ni miongoni mwa viongozi wa kiislamu watakao hutubia kongamano hilo, huku wengine wakiwemo, wahadhiri na wasomi kutoka Mombasa, Masheikh Yussuf Abdow, Abu Qatada, Sheikh Msellem na Sheikh Sugow.
Viongozi kadhaa kutoka kaunti za Mombasa, Kwale, Kilifi, Nairobi, Taita-Taveta, Lamu, Tana-River, Garissa, Wajir miongoni mwa nyengine wamehudhuria kongamano hilo.

 

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287