Bunge la Seneti kuamua hatma ya gavana Martin Wambora

Bunge la seneti, siku ya jumanne linatarajiwa kufanya kikao maalum kujadili hatma ya gavana wa Embu Martin Wambora ambaye alitimuliwa na bunge la kaunti juma lililopita.
Maseneta ambao wako likizoni, wameitwa na spika Ekwe Ethuro kujadili hoja hiyo muhimu ambayo endapo itapitishwa basi kiti cha ugavana kaunti ya Embu kitatangazwa kuwa wazi.
Wambora aliregeshwa madarakani na mahakama mwezi uliopita baada ya kubanduliwa madarakani na bunge la kaunti, hatua iliyoidhinishwa na bunge la seneti mwaka uliopita.
Tayari Wambora amekwenda mahakamani kupinga jaribio hilo la pili la kutaka kumng’oa.
https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287