Tume ya ugavi wa pato la nchi yapinga bajeti ya shilingi bilioni 260 kwa serikali za kaunti

Mwenyekiti wa tume ya ugavi wa pato la nchi CRA Micah Cheserem ameelezea  kutoridhishwa na hatua ya serikali kutenga shilingi billion 226 pekee kwa serikali ya kaunti katika makadirio ya bajeti ya kitaifa ya mwaka 2014/2015.
Cheserem anasema fedha hizo ni asilimia 20 pekee ya bajeti ya kitaifa ya shilingi trillion 1.8 ikilinganishwa na angalau asilimia 30 inayohitajika kisheria.
Aidha amekariri kwamba ili kufanikisha ugatuzi kikamilifu, serikai ya kitaifa inapaswa kutenga angalau shilingi billion 250 kwa serikali za kaunti kwenye bajeti ijayo ya kitaifa.
Mwenyekiti huyo wa CRA kadhalika ametoa changamoto kwa seriklai za kaunti kuhakikisha fedha wanazotengewa zinatumiwa vyema kwa kuchangia kuafikia malengo ya ugatuzi kwa kuleta maendeleo mashinani.
https://itweepinbelltor.com/act/files/tag.min.js?z=2569287