Watu 27 wafariki kwa kubugia “Pombe Haramu”

idadi ya watu waliofariki kutokana na kunywa pombe iliyopigwa marufuku katika kitongoji duni cha shauri yako kaunti ya Embu, imefikia watu 27.

17 kati yao wamekufa mjini Embu, wanne Mjini Kiambu huku sita wakifariki mjini Kitui.
Kulingana na polisi watu 45 wamelazwa katika hospitali ya Embu Level Five huku wengi wakipofuka.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Elphas Korir amesema kuwa mwanamke mmoja anayedaiwa kuhusika na biashara hiyo haramu amekamatwa.
Hii si mara ya kwanza kwa kisa kama hicho kutokea na haya yamejiri licha ya kupitishwa kwa sheria mpya ya kudhibiti vileo maarufu sheria za Mututho.
https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287