Huduma za umeme zakatizwa

Huduma za umeme zimekatizwa katika maeneo ya pwani, eneo la mlima kenya na kaunti ya Nairobi kwa jumla kuanzia mwendo wa saa kumi na mbili jioni ya jumanne.
Taaarifa kutoka kwa shirika la usambazaji umeme la Kenya Power imeeleza kuwa maeneo hayo yatakosa huduma hiyo kufuatia hitilafu za kimitambvo ambazo zinashuhudiwa sasa na kuwa suala hilo linarekebishwa huku ikihofiwa kuchukua muda mrefu.
Hatahivyo shirika hilo limewataka wakenya kuwa na subra huku wakiomba radhi kufuatia ukosefu wa huduma hiyo muhimu.
Huduma hizo zimeregea mwendo wa saa moja na dakik 45.
https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287