Mahakama ya juu yasimamisha uchaguzi mdogo wa Mathare

MAHAKAMA ya Juu imesimamisha kwa muda uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Mathare ikisubiri kusikizwa na kuamuliwa kwa rufaa ya aliyekuwa mbunge George Wanjohi.

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC ilikuwa imetenga tarehe tatu mwezi Jumi mwaka kuwa tarehe ya uchaguzi huo baada ya spika wa bunge Justin Muturi kutangaza kiti hicho kuwa wazi.

Juma lililopita mahakama hiyo ilitoa agizo sawia na hilo kusitishwa kwa uchaguzi wa Othaya hadi pale kesi iliyowasilishwa na aliyekuwa m bunge wa eneo hilo Mary Wambui itakapaoamuliwa..

Vile vile mahakama ya juu jana iliongeza muda wa kusimamishwa uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Othaya ambao ulistahili kufanyika hapo jana.

 

https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287