Afisa wa polisi aliyezua mjadala kwa kuvalia nguo ya kubana hataadhibiwa

AFISA wa polisi mwanamke ambaye  alizua mjadala mkubwa kwenya mitandao ya kijamii na hata kukashifiwa na wakubwa wake kwa kuvalia sketi fupi akiwa kazini hatachukuliwa hatua za kinidhamu.

Inspekta Mkuu wa Polisi David Kimaiyo amesema kuwa afisa huyo  Linda Okello hatachukuliwa hatua za kinidhamu kwakuwa suala hilo ni la kiusimamizi na kwamba afisa huyo tayari ametakiwa kuvalia suruali ndefu ili kuonekana nadhifu kazini, sambamba na kanuni inayofafanua jinsi maafisa wa polisi wanapasa kuvalia wakiwa kazini.

Kimaiyo alikuwa akimjibu Mbunge wa Mbita Millie Odhiambo aliyeelezea hofu kwamba huenda afisa huyo anayehudumu katika eneo la Lari, kaunti ya Kiambu, akaadhibiwa baada ya picha zake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zikionyesha akiwa amevalia sketi fupi na inayobana.

Kimaiyo alikuwa akijibu maswali  juu ya kashfa ya kuingizwa sukari humu nchini kiharamu, kutoka kwa Kamati ya Bunge kuhusu Kilimo ambayo Mbunge Millie Odhiambo ni mwanachama.

Kumekuwa na tetesi kuwa  huenda afisa huyo akahamishwa hadi katika eneo la Kaskazini Mashariki, penye changamoto za kikazi, kama njia ya kumwadhibu, madai ambayo Kimaiyo ameyakanusha.

https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287