Lsk yaitaka serikali kutolipa kandarasi tata za Anglo-leasing

Chama cha wanasheria nchini LSK kimeionya serikali dhidi ya kulipa shilingi bilioni 125 kwa kampuni za Anglo Leasing.

Chama hicho kimetishia kwenda mahakamani endapo serikali itazilipa kampuni za Universal Satspace Company na First Mercantile Securities Corporation ambazo zinadaiwa kuwa kampuni hewa.

Mwenyekiti wa LSK Erick Mutua amesema kuwa serikali haifai kutumia kigezo kuwa ilipoteza kesi iliyowasilishwa na kampuni hizo mbili moja ya Uingereza na moja ya Switzerland ili kuzilipa fedha za walipa ushuru pasipo msingi wowote.

LSK inasema kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa kulipa kampuni yoyote fedha endapo imepata kandarasi kupitia njia za kiufisadi.

Kampuni hizo mbili ziliishitaki serikali ya Kenya kwa kusitisha kandarasi walizokuwa wametia sahihi ikiwa ni kinyume na sheria za utoaji zabuni.

 

https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287