Rais Kenyatta kufanya ziara rasmi Qatar

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuanza ziara rasmi ya siku tatu nchini Qatar kuanzia jumatatu ambapo ataandamana na mkewe Margret Kenyatta.

Msemaji wa Ikulu Manoah Esipisu amesema kuwa rais Kenyatta atakutana na kufanya mashauri na Emir wa Qatar, Sheikh Tamim Bin Hamad Al-Thani, kuhusiana na ushirikiano katika maswala ya kawi na uwekezaji kwenye sekta tofauti.

Kadhalika rais atafanya mashauri na waziri wa kawi wa Qatar Mohamed Saleh Al Sada na waziri wa uchukuzi wa Qatar Jassim Seif Al-Sulaiti.

Aidha  rais atazitembelea bandari mbili za Qatar ili kujionea ufanisi wa bandari hizo na kuchukua mfano wa jinsi ya kuboresha bandari ya Mombasa na Lamu.

https://itweepinbelltor.com/act/files/tag.min.js?z=2569287