Mahakama yamrudisha Wambora mamlakani

Mahakama kuu ya Kerugoya imemregesha mamlakani gavana wa Embu aliyetimiliwa  Martin Wambora.
Majaji Boaz Olao, Hedwing Ong’undi na Cecilia Githua wamesema kuwa wabunge wa kaunti ya Embu na lile la Seneti walikiuka sheria kwa kujadili hatma ya Wambora ilhali mahakama ilikuwa imetoa agizo kusimamisha mijadala hiyo.
Kadhalika spika wa bunge la kaunti ya Embu ametakiwa kufika mahakamani kujibu shtaka la kupuuza agizo la mahakama.
Mahakama hiyo imesema hatua ya kumtaka gavana kufika mbele ya bunge la seneti ingefaa kuchukuliwa kama hatua ya mwisho endapo mazungumza kati yao yangekosa kuafikiwa.
Kwengine tukisalia  mahakamani, ni afueni kwa seneta maalum Naisula Lessuda baada ya mahakama ya rufaa kusema kuwa uteuzi wake ulifanywa kihalali.
Mahakama hiyo aidha imesema kuwa kupitia kipengee ya usawa wa maeneo nchini Lessuda anastahili kuwa katika wadhfa huo.
https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287