Wabunge wapinga uamuzi wa Mahakama kwenye kesi ya JSC

Mzozo wa kupimana ubabe kati ya wabunge na idara ya mahakama umeendelea kutokota baada ya kundi moja la wabunge kupinga uamuzi uliotolewa na mahakama kuu kulizuia jopo lililoteuliwa na rais kuwachunguza makamishena wa tume ya idara ya mahakama JSC.
Mbunge wa Ol Jorok John Waiganjo amesema kuwa wabunge watakwenda katika mahakama ya juu zaidi kutaka ufafanuzi wa kikatiba kuhusiana na majukumu ya bunge na idara ya mahakama.
Mbunge wa Mukurweini Kabando wa Kabando amesema kuwa idara ya mahakama haitakubaliwa kuwazuiya wabunge kutekeleza majukumu yao.
Mahakama kuu ilipitisha uamuzi kulizuia jopo maalum lililoteuliwa na rais Uhuru Kenyatta kuwachunguza makamishena sita wa tume ya huduma za idara ya mahakama JSC.
Majaji wa mahakama hiyo walisema katika uamuzi wao wa pamoja kuwa tume ya JSC, haiwezi kushurutishwa na bunge katika utenda kazi wake.
Kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa mahakamani na makamishena sita wa tume ya JSC baada ya bunge kupitisha hoja kutaka kuwaondoa mamlakani kwa utumizi mbaya wa mamlaka.
https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287