Likoni 1 ndio mabingwa wa Dola Super Cup Mombasa Edition.

Timu ya Likoni 1 ndio mabingwa WA Dola super Cup Mombasa edition

Hii ni baada ya timu hiyo kuilaza Likoni 2 mabao 6-5 kupitia mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja katika dakika 90 za mchezo katika uwanja WA Mwahima kaunti ya Mombasa.

Baada ya sare ya 1-1 dakika 90 za mchezo, na ushindani mkali ulijitokeza katika upigaji penanti kila timu ikitia kimyani penalty zake 5 za kwanza.

Hata hivyo shujaa wa ngarambi hiyo alikuwa ni Kipa Likoni 1 aliyewanyima wapinzani ushindi baada ya kupangua penalty ya ziada ya Said Abdallah wa Likoni 2 huku kiungo matata wa Likoni 1 Marco Cena akiitumia nafasi hiyo kuweka mkwaju wake wavuni na kuipatia timu yake ushindi.

Akizungumza baada ya michuano hiyo mkuu wa kitengo cha mauzo katika kampuni ya Dola Sadam Suleiman ambao ndio wadhamini wakuu wa Michuano hiyo, amesema kuwa lengo lao la kutambua na kukuza vipaji katika kaunti ya Mombasa limefanikiwa huku akiwa na imani kuwa baadhi ya wachezaji wa michuano hiyo watachukuliwa kucheza katika baadhi ya timu katika ligi kuu na zile za madaraja ya juu kuendelea kukuza talanta zao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Mombasa County Football Association Goshi Juma Ally amewataka wadhamini nchini kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha wanakuza vipaji vya vijana ili kukumbatia kandanda kama njia moja wapo ya kujipatia riziki.

Goshi ameomba kuimarishwa kwa viwanja ili kutoa nafasi ya vijana zaidi kukuza vipaji.

Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharif Nassir amewashkuru wadhamini wa michuano hiyo Dola kwa juhudi zao za kukuza talanta huku akiahidi kuimarisha hali ya viwanja katika kaunti ya Mombasa.

Abdulswamad akisema wanafanya kila juhudi ili kumaliza kujenga uwanja wa manuspaa ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kiwanja hicho kuchezewa AFCON.

Likoni 1 ambao ndio Mshindi wa michuano ya Dola Makala ya Mombasa alitia kibindoni shilingi laki 1 na sasa ataingia katika droo ya timu 8 bora kuwania ubingwa wa Pwani, ambapo Michuano sawia inaendelea katika kaunti zote 6 za pwani.

Msihindi wa jumla atatia kibindoni shilingi milioni 1.

https://phicmune.net/act/files/tag.min.js?z=2569287