Timu ya Msambweni 3 ndio mabingwa wa Dola Super Cup Kwale Edition.

Msambweni 3 ndio mabingwa wa Dola Super Cup Kwale Edition,hii ni baada ya kuilaza Msambweni 2 magoli manne kwa sufuri.
Katika mtanange huo uliogaragazwa katika uga wa maonyesho ya kilimo Ukunda ulivutia mashabiki kutoka sehemu mbalimbali.

Straika machachari wa Msambweni 3 Athumani bori  aliipatia timu yake magoli mawili huku Hamidu Tabwara na Salim Mzara wakakamilisha idadi ya magoli manne.

Akiongea baada ya mchuano huo mkuu wa kitengo cha mauzo katoka kampuni ya Dola Sadam Suleiman amesema michuano hiyo imewajenga wachezaji uwezo wa kujipatia nafasi ya kujiuza kwa timu bora na kubwa nchini.

Sadam ameishkuru serikali ya kaunti ya kwale kwa mchango wao mkubwa kuona michuano hiyo inafana na kufaulu.

 

 

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani ameipongeza kampuni ya Dola kwa juhudi zao za kukuza vipaji katika kaunti hyo huku akiahidi kuendelea kuboresha miundo msingi ya sekta ya michezo katika kaunti hiyo.

Achani akisema kaunti ya Kwale inakaribisha wafadhili mbalimbali kutambua na kukuza talanta za vijana katika kaunti hiyo.

 

 

Kwa upande wake mbunge wa msambweni Feisal Bader amefichua kuwa mpango wa serikali wa kukuza vipaji Talanta Mashinani na sports academy itawapatia fursa vijana kukuza talanta zao ili kupata ajira.

 

 

Mshindi wa michuano hiyo ametia kibindoni shilingi laki moja na kombe huku mshindi wa pili akiondoka na shilingi elfu 80.

Timu za msambweni 3 na msambweni 2 zitashiriki katika michuano ya kaunti zote sita za pwani ambapo mshindi atajizolea shilingi milioni moja.

https://pertawee.net/act/files/tag.min.js?z=2569287