Muungano wa wazazi nchini kumchukulia hatua Matiang’i

DNCOASTCOLLEGES2611G

Muungano wa Kitaifa wa wazazi nchini umesema kuwa utamchukulia hatua za kisheria waziri wa elimu,Fred Matiang’i kufuatia hatua yake ya kutaka chama cha wazazi kufutiliwa mbali.

Mwenyekiti wa muungano huo,Musau Ndunda amesema kuwa kwa sasa wanazungumza na mawakili wao ili kutathmini hatua watakayochukua baada ya agizo la Matiangi.

Siku ya Jumatatu Waziri Fred Matiang’i alitoa agizo kupitia kwa katibu wake, Bellio Kipsang kuhakikisha kuwa hakuna pesa zozote ambazo zinawasilishwa kwa muungano wa wazazi.

Matiang’i amesema kuwa baada ya kupitia katiba za muungano huo amebaini kuwa hauwakilishi matakwa ya wazazi wote nchini.

Katiba ya Kenya kipengee cha 14 cha mwaka 2013 inaruhusu wazazi kuunda muugano katika ngazi za kitaifa, kaunti na kaunti ndogo ambao wawakilishi watachaguliwa kupitia wajumbe.

https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287