Waziri wa fedha atakiwa kueleza taratibu zilizotumika kuhamisha Eurobond

images (1)

Mbunge wa Mugirango Kusini Manson Nyamweya amemtaka waziri wa fedha Hennry Rotich kuweka wazi taratibu zilivyofuatwa katika juhudi za kuhamisha fedha eurobond kutoka banki ya marekani hadi banki kuu.

Nyamweya amesema stakabadhi hiyo itakuwa njia pekee ya serikali kujitetea kutokana na madai ya kufujwa kwa pesa hizo.

Nyamweya hata hivyo amemsuta waziri Rotich kwa kutoonesha uzalendo kwa kufungua akaunti nyingine Marekani ya kuhifadhi pesa hizo badala ya kuruhusu fedha hizo kuhamishwa moja kwa moja hadi benki kuu ya Kenya.

https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287