Rais Kenyatta akutana na Riek Machar

riekj

Rais Uhuru Kenyatta amefanya mashauriano na aliyekuwa naibu rais wa Sudan kusini Riak Machar katika ikulu ya rais, jijini Nairobi.

Machar amemfahamisha rais Kenyatta kuhusiana na mazungumzo yake na mwenyekiti wa mamlaka ya serikali za kanda hii kuhusu maendeleo IGAD ambaye ni waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn,hususan katika juhudi za kuleta amani katika taifa hilo.
Machar amemsifu rais Kenyatta na waziri mkuu wa Ethiopia kutokana na juhudi zao za kuleta amani katika taifa hilo linalokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Aidha kiongozi huyo ameelezea kujitoleea kwa upande wake katika mazungumzo ya kuutafutia ufumbuzi mzozo unaolikumba taifa hilo.