TUTAKOMESHA UNYAKUZI WA ARDHI,YASEMA TUME

Swala la ardhi limekuwa donda sugu hususan maeneo ya pwani, jambo ambalo limesababisha migogoro kuibuka kati ya wananchi na kuwapa viongozi mda mgumu kutatua.
 Mwenyekiti wa Tume ya ardh Mohamed Swazuri amesema kuwa tayari mikakati kabambe imewekwa ili kutatua matatizo ya ardhi  katika maeneo mbali mbali nchini ikiwemo Ngomeni, kwale,Shikaadabu na ziwa la ng’ombe.
 Aidha Swazuri ameeleza kuwa wengi wa wakazi katika kanda ya Pwani wanamiliki vyeti vya ardhi  lakini sio wamiliki asili ya ardhi hizo.
 Swazuri ameeleza kuwa atashirikiana na serikali za kaunti kuwapa vyeti vya ardhi maskuota waliokatika fuo za bahari na sehemu zengine.
Radio Salaam News
www.salaamfm.com
https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287