Mzozo kati ya Pussetu na Cotu waendelea kutokota

Mzozo kati ya muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU na ule wa wafanyikazi wa umma PUSSETU unazidi kutokota huku kila mwamba ngoma akivutia upande wake.

Pusetu imekashifu vikali hatua ya COTU kulipia viwanja na kumbi zote ambapo sherehe za leba dei zilitarajiwa kufanyika.

Naibu mwenyekiti wa PUsetu Sammy Kubasu amesema kuwa sherehe za leba dei si za COTU pekee na licha ya hatua hiyo hawatakosa kuhudhuria sherehe hizo.

Kubasu amesisitiza kuwa maandalizi ya sherehe hizo hayafai kuonekana kama mzozo kati ya miungano hiyo mikuu ya wafanyikazi nchini na wananchi wote wanapaswa kushiriki katika siku hiyo.

https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287