MAHAKAMA YAKATAZA BUNGE LA KAUNTI YA NAIROBI KUMFUKUZA WAZIRI  WA UCHKUZI.

countyBunge la kaunti la Nairobi limezuiliwa na mahakama kusitisha zoezi la kuondoa mamlakani waziri wa barabara wa kaunti hiyo Evans Ondieki.
Jaji wa Mahakama hiyo Isaack Lenaola amemzuia gavana wa Nairobi, Evans Kidero kumfuta kazi Ondieki kutokana na pendekezo la bunge la kaunti hiyo.
Lenaola ameongeza kuwa iwapo bunge hilo litapitisha hoja ya kumsimamisha kazi waziri huyo, zoezi hilo  litaweza batilishwa na mahakama.
Wabunge wa kaunti hiyo wamedai kuwa Ondieki amehongwa  ili afunge mradi wa basi za kaunti itakayopunguza  nauli na kufaidisha wananchi.
Na Ibtisam Jamal.
https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287