Maafisa wawili wa polisi wauawa kwenye mlipuko Nairobi.

Maafisa wawili wa polisi ni miongoni mwa watu wanne waliofariki jana usiku kufuatia mlipuko uliotokea katika eneo la Pangani Jumatano usiku.
Mlipuko huo unadaiwa kutokea wakati polisi walipokuwa wakiwapeleka washukiwa kwenye gari moja walilolikamata kwenye kizuizi cha Pangani.
Gari la washukiwa hao lililipuka baada ya kukaribia kituo cha polisi cha Pangani na wote wakafariki pamoja na maafisa wawili wa polisi waliokuwemo ndani ya gari hilo.
Kadhalika gari la polisi lililokuwa likifuata lile la washukiwa hao liliharibiwa na mlipuko huo.
Inspekta Jenerali wa polisi David Kimaiyo ambaye alizuru eneo la tukio amesema kuwa shambulizi hilo halitatatiza juhudi za kiusalama zinazoendelea hivi sasa.
Kadhalika waziri wa mambo ya ndani Joseph Ole Lenku alizuru eneo hilo.
Mlipuko huo unajiri huku polisi wakiendeleza msako mkali dhidi ya washukiwa wa uhamiaji haramu na wahalifu wengine kote nchini.
https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287