Familia elfu moja Kinango zanufaika na msaada wa Chakula kutoka kwa KPA

HALMASHAURI ya bandari nchini KPA imetoa msaada wa chakula uliyogharimu  jumla ya shilingi milioni 1.5 Kwa familia zinazokumbwa na baa la njaa Katika eneo Bunge la kinango Kaunti ya Kwale.

Msaada huo ulitolewa Kwa familia  zisizojiweza Katika maeneo ya Ndavaya na Lutsangani ambayo yameathirika vibaya kutokana na janga la ukame.

 

Mwenyekiti wa bodi ya KPA Benjamin Tayari aliongoza zoezi la kutoa msaada huo wa chakula  Kwa familia elfu moja zilizoathirika Katika maeneo hayo.

Akizungumza Wakati wa zoezi hilo Tayari alidokeza kuwa maeneo mengi ya Kaunti ya Kwale bado yamesalia kame kutokana na ukosefu wa mvua ya kutosha, huku akisema halmashauri ya KPA itahakikisha  wahanga wa janga la  ukame ambao wanahitaji msaada wa chakula Kwa dharura wanasaidiwa.

Mwenyekiti huyo Hatahivyo alionyesha masikitiko yake na jinsi janga la ukame nchini lilivyosababisha vifo na kuchangia idadi kubwa ya watu kuyahama makaazi yao.

 

Ameongeza kusema kuwa halmashauri ya KPA inafanyakazi Kwa karibu  na serikali ya kitaifa na zile za Kaunti ili kusaidia kukabiliana na mgogoro wa kibinadaamu ambao umesababishwa na kipindi kirefu cha ukame kinachoendelea kushuhudiwa sasa.

Vile vile amezihakikishia jamii za eneo Hilo kuhusu kujitolea Kwa halmashauri ya KPA katika kuangazia mahitaji Yao ya chakula Wakati wa dharura kupitia kitengo cha wajibu wa kiraia cha mamlaka hiyo (CSR).

Mwenyekiti huyo alikuwa ameandama na wafanyikazi wengine wa KPA wakiongozwa na meneja wa mawasiliano wa halmashauri hiyo Bernard Osero ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji wa jamii Katika mamlaka ya KPA.

Kwa upande wake akizungumza Wakati wa mkutano huo Naibu Kaunti kamishna wa eneo Bunge la Kinango Abdullahi Galgalo aliishukuru KPA Kwa msaada huo iliyoutoa.

Aliongeza kusema kuwa eneo Hilo Lina takriban watu elfu thelathini na nane ambao wengi wao wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula.

 

Naye Mwakilishi wadi wa Ndavaya Ali Beja vile vile aliishukuru KPA Kwa msaada huo, huku akiiomba halmashauri hiyo kufadhili uchimbaji wa visima vya maji Katika eneo Hilo.

Kulingana na kamati Shirikishi ya kukabiliana na ukame Katika Kaunti ya Kwale Takriban watu laki mbili Katika maeneo ya Kinango,Shimba Hills,Samburu na Lunga Lunga wako Katika uhitaji wa dharura wa chakula cha msaada na maji

https://upskittyan.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287