Wanahabari wafaidika na mafunzo ya mabadiliko ya tabia nchi.
Waandishi kutoka ukanda wa pwani wafaidika na mafunzo ya kuangazia maswala ya mabadiliko ya tabia nchi yaliyoandaliwa na muungano wa wahariri nchini kwa ushirikiano na shirika la GIZ.
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliwajenga uwezo waandishi na kupata elimu huku serikali kupitia msemaji wake ikiaahidi kushirikiana nao kuangazia maswala ya mabadiliko ya tabia nchi.
Akiongea katika warsha hiyo msemaji wa serikali nchini Isaac Mwaura amesema ofisi yake ikishirikiana na wizara ya mazingira itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha ushirikiano mwema kati ya KEG NA GIZ kwa kuwawezesha waandishi kupata elimu ya mabadiliko ya tabia nchi.
Mwaura akisema anatizamia kufanya kazi na waandishi kote nchini kupitia vilabu vyao uli kuweka uhusiano mwema kati ya serikali na waandishi wa habari.
Kwa upande wake muwakilishi kutoka wizara ya mazingira nchini Temesi Mukami amesema warsha hiyo imekuwa yakufana haswa katika kubaini changamoto pamoja na mapendekezo ambayo yatasaidia pakubwa waandishi katika kuandika na kuripoti maswala ya mabadiliko ya tabia nchi.
Temesi akisema watabuni mtaala maalum ambao utatumika na taasisi mbalimbali za mafunzo pamoja na waandishi katika maswala ya mabadiliko ya tabia nchi.
Martin Masai mmoja wa muamana (trustee) wa KEG amesema wao kama muungano wapo tayari kushirikiana na kufanya kazi na kila mtu kuhakikisha wanafanikiwa kutimiza malengo yao.
Akisema wanataka kuwaelemisha wananchi ni jinsi gani vyombo vya habari zinafanya kazi ili kuwa rahisi kuhakiki ufanya kazi wa serikali.