Serikali na taasisi za fedha zatakiwa kuhusisha wananchi Katika maswala la fedha

Picha ya afisa mkuu mtendaji wa Shirika la Transunion Kenya Morris Maina.

NA ELNORA MWAZO

AFISA mkuu mtendaji wa kampuni ya Transunion Kenya Morris Maina amesisitiza haja ya serikali na taasisi nyengine za fedha ulimwenguni kuhusisha wananchi Katika sekta ya fedha kwa kuwaelimisha maswala mbalimbali yanayoihusu sekta hiyo.

Akizungumza na wanahabari Mjini Mombasa katika kongamano la sita lililowaleta pamoja wadau wa sekta hiyo liloingia siku yake ya tatu hii Leo, afisa huyo mkuu mtendaji amesema kuwa endapo wananchi wataelimishwa kikamilifu maswala ya fedha, itawawezesha pakubwa kuimarisha maisha Yao na hivyo kuchangia ukuaji wa kiuchumi wa mataifa yao.

Amesema kama kampuni ya transunion Kenya wamekuwa wakitoa elimu Kwa wananchi kufahamu rikodi zao za kifedha ili kuwawezesha kupata mikopo Kwa urahisi.

Picha ya afisa mkuu mtendaji wa Shirika la Transunion Kenya Morris Maina.

Wakati huo huo ameipongeza hatua ya banki kuu hapa nchini CBK kuweka Sera mbadala za Kudhibiti mikopo inayotolewa na kampuni mbalimbali kupitia simu za mkononi,akidokeza kuwa kama kampuni ya maswala ya fedha wamebuni huduma zinazokabiliana na ulaghai unaondeshwa kupitia mitandao.

Vile vile ameupongeza uvumbuzi wa kidijitali Katika sekta hiyo uliyofanywa Katika miaka ya karibuni akitoa mfano wa hazina ya hustler fund ambayo amesema imewezesha pakubwa wakenya wengi mikopo Kwa urahisi.

 

 

https://phicmune.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287