Inspekta Jenerali wa polisi Japhet Koome akosa kuhudhuria kikao cha kamati ya bunge ya utekelezaji wa katiba,Washinikiza Kumtimua.

Wabunge katika kamati ya utekelezwaji wa katiba wameeleza kutofurahishwa kwao na hatua ya inspekta jenerali wa polisi nchini Japhet Koome kwa  kutohudhuria kwake kikao kilichoitishwa na kamati hiyo.

Wakiongea na waandishi wa habari katika kaunti ya Mombasa wabunge hao wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Gathoni wamuchomba,wamesema walitarajia Koome kuhudhuria na kujibu tuhma zinazomuandama kuhusu utendakazi wa Tume ya HUduma za polisi NPSC, zikiwemo kutumia mamlaka yake kinyume na sheria.

INSERT -TUHUMA ZA KOOME

 

Aidha Wamuchomba amesema Koome amekuwa akifanya kazi  pasi kuzingatia majukumu yake kikatiba wala kufanya mikutano na makamishna wa tume ya Huduma za Ppolisi kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maafisa wa polisi.

 

 

Kwa upande wake mbunge wa kibwezi Mashariki Jesica Mbalu ambaye ni  mmoja wa wanachama wa kamati hiyo   amesema kutokana na uchunguzi wao Koome anahujumu utendakazi wa Tume ya huduma za polisi hasa kwa kukosa kuhudhuria mikutano anayofaa kuonana na tume ya huduma za polisi inayolenga kuzungumzia mustakabali wa utendakazi wa polisi.

 

 

Kamati hiyo sasa wanamtaka koome kuhudhuria kikao hicho ili kujibu tuhma zinazomkali la sivyo itashinikiza kubanduliwa kwake kama inspekta jenerali wa polisi kwa kile wanachokisema kutozingatia sheria

 

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287